Tuesday 3 July 2018

Jinsi ya kupika pilau ya nyama ya kuku, ng'ombe au mbuzi

[​IMG]

Mahitaji
  • 240 gram za mchele
  • 240 gram za nyama iwe ya kuku au ng'ombe au mbuzi kata katika umbo dogo la kutosha kula. Ili nyama yako iwe laini chukua papai lililoiva baada ya kukatakata nyama pondea papai katika bakuli lenye nyama kisha weka chumvi kidogo, soya sauce kidogo, kitunguu swaumu na tangawizi kwa ladha zaidi. Nyama hii iweke kwenye friji kwa dakika 45 tu iwe ndani katika mchanganyiko huu itakua laini sana na utaipika kwa muda mfupi.
  • 1 kijiko kidogo cha chai mbegu za binzali nyembamba (cumin seed)
  • 1 kitunguu kikubwa kata kata
  • Nyanya kubwa kata kata
  • 3 spring onions (majani ya kitunguu)
  • 1 bay leaf
  • 3 cloves (Mbegu za Karafuu )
  • 3 cardamom ( mbegu za hiriki)
  • 1/2 kijiko cha chai kidogo turmeric powder ( Unga wa manjano)
  • 5 gram kitunguu swaumu
  • 1 pilipili mbuzi kata kata
  • 5 gram unga wa tangawizi au ya kusagwa
  • 1 kijiko kidogo cha chai garam masala
  • 600 gram coconut milk (Tui la nazi) sio lazima kama hutumii nazi basi weka maji kawaida
  • 5 gram chumvi
  • 1 fungu la giligilani kwa jili ya kupambia
  • 1 kijko kidogocha chai maji ya limao (sio lazima)

Jinsi ya kupika
  1. Katika sufuria weka kijiko 1 kikubwa cha chakula mafuta kisha kaanga mbegu za binzali nyembemba, bay leaf, karafuu, mbegu za hiriki, kitunguu swaumu, pili pili mbuzi, tangawizi, nyama na chumvi kisha kaanga.
  2. Kitunguu kikishalainika weka nyanya pamoja na unga wa manjano na garam masala. Kaanga kwa dakika 2.
  3. Weka mchele hakikisha unauweka bila maji. Hakikisha una ugeuza geuza mpaka mchele ubadilike rangi na kutoa harufu safi baada ya kuukaanga.
  4. Ongeza tui la nzai au maji kwa wale wasio tumia nazi endelea kukoroga ichanganyik vizuri.
  5. Funika na mfuniko kisha pika kwa dakika 10 au mpaka mchele wako utakapoiva na kuwa wali.
  6. Kisha ugeuze wa chini uje juu na wajuu uende chini.
  7. Kwa kuipendezesha pilau yako sasa mwagia kwa juu majani ya kitungu na majani ya giligilani kisha nyunyizia kwa juu maji ya limao kwa sababu kuu mbili. Moja ni kuongeza ladha. Pili inasaidia kupunguza kiwango cha sodium.
  8. Kwa wale wapenda samli unaweza weka kijiko kimoja pia itaongeza harufu na ladha safi katika pilau yako.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...