Mahitaji
Kabichi 1/2 kilo
Nyanya ya kopo 1/2
Kitunguu 1
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Chumvi
Olive oil
Matayarisho
Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe
maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa
nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika
sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia
chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na
upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa
tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.
No comments:
Post a Comment