Friday, 10 August 2018

Chipsi zenye asali na pilipili


Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Kwa viazi vya kukaanga

Nusu kilo viazi
Vijiko 3 vya chakula corn flour/ corn starch
Chumvi kwa kuonja
Mafuta ya kukaangia

Kwa ajili ya sauce

Kijiko 1 cha chai tangawizi na kitunguu saumu
Vijiko 2 vya chakula asali
Kijiko 1 cha chakula mafuta ya kupikia
Kijiko 1 cha chakula sosi ya soya
Vijiko 2 vya chakula chili sauce
½ pilipili hoho nyekundu
Kijiko 1 cha chai hoisin sauce (ukipenda)
¼ kikombe majani ya kitunguu

Maelekezo

Menya, osha na katakata viazi umbo la chipsi; toa mbegu na katakata pilipili hoho vipande virefu vyembamba; katakata majani ya kitunguu vipande vyembamba; twanga tangawizi na kitunguu saumu
Kwenye bakuli kubwa, weka viazi na chumvi. Changanya vizuri, kisha ongeza corn flour, changanya vizuri
Chemsha mafuta kwenye kikaangio moto wa juu kiasi. Ongeza viazi, kaanga mpaka viive na viwe vya rangi ya kahawia. Kumbuka kugeuza mara unapoweka kwenye mafuta visishikane. Toa kwenye mafuta, chuja mafuta
Kwenye kikaango kingine, weka mafuta kijiko 1 cha chakula. Yakichemka ongeza kitunguu saumu na tangawizi. Kaanga kwa sekunde kama 30 kisha weka pilipili hoho uikaange kwa dakika kama 2 halafu weka majani ya kitunguu
Ongeza asali, hoisin sauce, sosi ya soya na chilli sauce. Kanga kwa dakika 1 nyingine
Ongeza viazi vilivyokaangwa. Changanya vizuri sosi ikolee kwenye viazi
Pakua cha moto

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...