Wednesday, 8 August 2018

Unajua Makande ya mahindi mabichi na nazi??


Maandalizi; dakika 5
Muda wa kupika; dakika 35
Muda jumla; dakika 40


Mahitaji



Vikombe 1½ mahindi mabichi yaliyochemshwa
Kikombe 1 maharagwe yaliyochemshwa
½ kikombe tui la nazi
Kijiko 1 cha chai beef/ chicken/ vegetable boulloin powder
Nyanya 1 ya wastani
Kitunguu 1 kidogo
¼ kijiko cha chai kitunguu saumu (Ukipenda)
Kijiko 1 cha chai mafuta ya kupikia (ukipenda)
½ kikombe ham iliyokatwakatwa (ukipenda)
Chumvi kwa kuonja

Malekezo

Weka kitunguu na nyanya kwenye mashine ya kusagia chakula kutengeneza rojo. Endapo hutatumia mashine, unaweza pia kukwangua au kukata vipande vidogovidogo sana



Kwenye sufuria katika moto wa wastani, weka maharagwe, rojo ya nyanya, bullion powder, kitunguu saumu, mafuta na kikombe kimoja cha maji (KAMA MAHINDI YAKO SIYO MALAINI SANA, WEKA MAHARAGWE NA MAHINDI PAMOJA)



Funika na mfuniko, acha iive taratibu kwa moto wa chini kwa dakika 20, endapo maji yatakaukia, ongeza maji zaidi



Hakikisha kila kitu kimeiva vizuri



Ongeza tui la nazi, pika kwa dakika 5 nyingine



Ongeza mahindi na maji zaidi ikibidi, pika dakika 10 nyingine. Ongeza chumvi ikihitajika



Kaanga ham kwenye kikaangio moto wa juu



Pakua kande kwenye bakuli, weka ham kwa juu. Mwagia na majani yoyote utakayopenda kuremba kande zako



Iliwe ikiwa ya moto

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...