Sunday 30 September 2018

JIFUNZE KUPIKA SWAHILI: Chips na kuku



Chips zilizochanganywa na kuku, chakula hiki ni kizuri na rahisi kuandaa. Radha ya chakula hiki ni nzuri sana na utafurahia.

Kuandaa: dakika 15
Mapishi: dakika 45

Mahitaji
 Kuku ½ kg
Viazi ulaya ½ kilo
Nyanya 2 kubwa zilizoiva vizuri
Kitunguu saumu ¼ kijiko cha chai
Tangawizi ¼ kijiko cha chai
Korianda ¼ kijiko cha chai
Hing ¼ kijiko cha chai
Chumvi ½ kijiko cha chai
Pilipili manga kijiko 1 cha chai
Mafuta ya kula
Apple cider vinegar ½ kikombe cha kahawa
Oyster sauce vijiko 2 vya chakula
Kitunguu maji 1

Maelekezo
Menya viazi kisha kata ukubwa wa chips unaopenda. Hifadhi vizuri kwenye maji yaliyowekwa chumvi.
Safisha kuku vizuri kisha weka kwenye sufuria safi. Mwagia vinegar juu ya kuku. Bandika sufuria ya kuku jikoni. Acha ichemke vizuri. Kisha toa na hifadhi pembeni.
Bandika kikaango, weka mafuta ya kula. Mafuta yakipata moto weka viazi na kaanga hadi chips ziive. Epua na hifadhi pembeni. Rudia hadi viazi vyote viwe vimepikwa.
Kaanga kuku kwenye mafuta uliyotumia kupikia chips.
Bandika sufuria jikoni, weka mafuta. Yakipata moto weka kitungu maji na viungo vyote ila usiweke nyanya na oyster sauce. Vitunguu vikianza kubadilika rangi weka nyanya. Nyanya zikiwa tayari weka kuku na funika vizuri kwa dakika 5 kisha weka oyster sauce. Ongeza supu ya kuku nusu kikombe kwenye sufuria, acha ichemke.
Weka chips kwenye sufuria lenye sauce ya kuku, pika hadi supu ikaukie.
Epua, tenga chakula na jirambe.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...