Tuesday 2 October 2018

JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA KATLESI ZA SAMAKI.



Vipimo

Viazi - 5 kiasi

Tuna - 2 vikopo

Carrot - 1

Pilipili mboga - Nusu

Kitunguu saumu(thomu/galic) - ½ kijiko cha chai

Pilipili - kiasi

Chumvi - kiasi

Ndimu - kiasi

Unga wa ngano - ½ kikombe

Yai - 1

Mafuta ya kupikia - Kiasi

Namna ya kutayarisha na kupika

Menya Viazi uvichemshe na chumvi.

Vikiwiva vichuje maji, viponde ponde, vilainikie – weka kando

Chuna carrot ziwe kama chicha, kata pilipili mboga  nyembamba nyembamba, fungua vibati vya Tuna kamua majia yake mwaga.Changanya Tuna, carrot, pilipili mb

oga, thomu, pilipili kali, chumvi, ndimu, kisha uchanganye na viazi ulivyoviponda. Hakikisha vimechanganyika vizuri.

Tengeneza vidonge kiasi unachotaka na kata umbo unalopenda kama la yai au duwara ukimaliza weka pembeni.

Changanya unga na maji uwe mzito mzito tena uchanganye vizuri na yai.

Weka karai katika moto, mimina mafuta kama ya maandazi, kisha chukua vidonge chovya katika unga uliochanganywa yai  na utumbukize ndani ya mafuta yaliopashika moto vizuri.

Ziwache mpaka zibadilike rangu, uzitoe. Tayari kwa kula.

#mapishi #mapishigram #mapishiyetu
v_massalaAsante ,Ya yai me nataka jmn
middmach75@mrs_middmach
ackrina_kadiliAsante, mara ya mwisho nilipika katlesi za nyama ya kusaga, lkn nilitengeneza shimo katika nikaeka nyama ya kusaga, wakati wa kukaanga mafuta yalikua haya fiki katikati
annyjaycob3sawa sawa @mapishigram lakn io tuna ndo nn ?? naomba nieleweshe mmakonde mimi
ackrina_kadiliNitajaribu kwa namna hii, bt tuna kwangu itakua ngumu so I'll try nyama ya kusaga kwa namna hii. Asante kipenzi I appreciate ua good work
dadamzalendoNaomba na recipe ya cutless za viazi mpendwa
asha.ramahsamaki mbona sijaona unachanganya mdacgan
abiolaskids_jlovely

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...