Tuesday 2 October 2018

JINSI YA KUTENGEZA JUICE YA MCHANGANYIKO WA TIKITI NA LIMAO.


MAHITAJI
450 grams Vipande vya Watermelon vyenye ubaridi,
250 gram ya maji ya dafu au Nazi changa
1 limao kubwa
10 vipande vya barafu au Ice cubes,
Fresh Mint kwajili ya kupambia

Kata nusu tikiti maji zuri lililoiva kama unavyoona kwenye picha kisha likate kate vipande na uweke kwenye friji vipoe kabla ya kutengeneza juisi yako

Chukua maji ya dafu, limao, vipande vya barafu na vipande vya tikiti maji kisha weka kwenye blender. Lengo la kuweka limao ni kuongeza na kubalance ladha. kama wewe ni mpenzi sana wa maji ya madafu unaweza ongeza zaidi ili ladha ya madafu isikike sana.
Blend vizuri mpaka vitu vyote vichanganyike safi kabisa.

Perfect drink for your summer, waandalie familia wafurahie pia kama unabiashara waandalie wateja wako wafurahie sana hasa kipindi hiki cha majira ya joto. kumbuka tikiti maji na dafu vyote vinasukari kwahiyo huna haja ya kuongeza sukari kabisa na ukafurahia kinywaji hiki murua.
tarimkyeAsante

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...