Kutokana na kuwa na utumbo mdogo, watoto hawali sana.Ndio maana ni muhimu kuwa na uhakika wa chakula wanachokula kina lishe nyingi za kutosha na zote.Jifunze au jua jinsi ya kuweka muda wa kula kwa watoto ili wapate hizo lishe bora kwao.
Muda wa mzuri wa kula
Kiujumla,chakula cha nguvu ni kwa kuanzia watoto wa miezi sita (6)na kuendelea,pindi kinapoandaliwa zingatia akili ya ulaji wa mtoto wako.Lakini vizuri pia uzungumze na mkunga au daktari wa watoto kabla ya kumpa mayai,samaki,citrus,na maziwa ya mtindi kama mtoto wako mdogo chini ya mwaka kwasababu vyakula hivyo huweza kusababisha allergy.Vyakula vingine kama nyama,matunda,na mboga mboga huweza kuanza kumlisha mtoto wa miezi 6 .Ila kumbuka vyakula hivyo vya aina yoyote kisitambulishwe kwa mtoto wa miezi mine(4).
Japokuwa watoto hukua kwa utofauti,ni vizuri kutafuta ushauri wa daktari au watu wazima dawa wale, kwa kujihakikishia pindi unapotaka kumuanzishia chakula mtoto na pia kipi ni bora zaidi kwa huyo mtoto wako.
Ndizi
Ndizi zina wanga (carbohydrates) mwingi,amabayo hutia nguvu,vile vile fiber kwa kusuport kulainisha mmeng’enyo chakula tumboni.Ni kizuri na chepesi kuwa chakula cha mtoto,na huwa rahisi kuiva kwake.Pindi unapoandaa ndizi kwa mtoto mdogo,hakikisha imeiva vizuri na imepondeka vizuri.Kwa mtoto mkubwa anaweza kula ndizi kama ilivo yaani nzima,lakini iwe pia imeiva vizuri iwe rahisi kwa mtoto kuisaga na kuimeza kwa urahisi zaidi.
Viazi vitamu
Viazi vitamu ni kizuri chenye chanzo ya potassium, vitamin C, na fiber na wingi wa beta-carotene, ni antioxidant ambayo husaidia kulinda aina za magonjwa cancer na kusafisha free radicals.Watoto wengi hupenda viazi vitamu zaidi kuliko mboga mboga kwasababu ya ladha yake ya utamu wa asili.Pindi unapopika hivi viazi viponde au kusaga,viazi vitamu ina ulaini ambao ni rahisi kwa mtoto kuvila,hata kwa watoto ambao ndo wanaanzishiwa kula solids au vyakula vigumu.
Parachichi(avocado)
Parachichi wakati mwingine huwa kama mboga,lakini hilo ni tunda!Ina lishe nyingi kuliko aina ya vyakula vingine vifananavyo na parachichi.Parachichi lina protini nyingi katika mafungu ya matunda na ni tajiri wa mafuta (fat)-“ni nzuri” aina hii ya mafuta inavilinda vidudu au diseases vya ugonjwa wa moyo.Hakikisha unampa mtoto parachichi liloiva vizuri .Osha nje ya hilo tunda,kisha menya maganda na lisage liwe laini.Sababu lina mafuta mengi kwahiyo mara moja mtoto kushiba,mpe kidogo na chakula kingine,huweza kuwa kuku au nyama laini.
Mayai
Mayai ni mazuri.Yai leupe huwa ni protein tu na kiini kina zinc na vitamins A, D, E, na B12.
Kiini pia kina choline, research inaonyesha ni nzuri kwa afya ya maendeleo ya kukuza akili.Kimila,madaktari wa watoto huwa wanashauri walezi wasiwape watoto mayai—na sana sana ile nyeupe—mpaka baada ya mwaka kwa sababu ya matokeo ya alergy.
Lakini huo ushauri kwa sasa umebadilika,na baadhi ya wataalam wanaamini kwamba mayai yacheleweshwe kwa familia ambazo zina historia ya matatizo ya allergy.Wakati mayai ni chanzo kikuu cha protein na lishe nyingi nyingine,shauriana na mtaalam wako pindi mtoto wako ameanza kula vyakula kuangalia kama ni sawa au kipindi gani itafaa kumpa mayai mtoto wako.
Kwa upande wangu nashauri mayai mazuri ni ya kienyeji na sio ya kuku wa kisasa au kizungu kwa sababu ya dawa na muda wa utotolewaji wake pia ni mdogo.
karoti
karoti ina wingi wa beta-carotene, na antioxidant ambayo hutoa ile rangi ya orange.Beta-carotene hubadilishwa kuwa vitamin A mwilini na huchukua nafasi ya kukuza ukuaji na afya ya kuona.Kupika karoti huleta ladha ya asili yake ya utamu,ambayo hupendwa na watoto sana,ambao wamezaliwa wanapenda ladha ya vitu vitamu.Unapoandaa karoti kwa mtoto mdogo,hakikisha zinaiva sana hadi kuwa laini.Kama mtoto mkubwa na anweza kula ikiwa nzima ilioiva haijalainika huwa nzuri zaidi,unaweza kumlisha ilopikwa kidogo tu.
Maziwa ya mtindi
Maziwa ya mtindi humpatia mtoto calcium, protein, na phosphorus,ambazo ni muhimu kwa kukamavu au kutia nguvu,mifupa yenye afya na meno. Maziwa ya mtindi yana probiotics,ni aina ya bacteria mzuri ambae anasidia katika mfumo wa usagaji chakula na kusupoti immune system. Watoto wanahitaji sana mafuta katika mlo wao,kwahiyo chagua maziwa mazuri ya mtindi ambayo yana mfuta kidogo,au yana aina ya mafuta tofauti tofauti .
Pia epuka maziwa ya mtindi ya ladha au flavored,ambayo huwa yana sukari nyingi.Kama unahisi kuongezea ladha,changanya na matunda yalosagwa.Mtoto chini ya umri wa mwaka huweza kuwa na matokeo mabaya ya protein inayopatikana kwenye maziwa ya mtindi,usisite kushauriana na daktari wa mtoto wako kabla hujampatia maziwa hayo .
Baby cereal
Iron-fortified infant cereals humpa mtoto wako madini ya chuma yanayotakiwa katika ukuaji wake. Watoto huzaliwa na madini ya chuma,lakini huanza kupungua au kuisha kuanzia miezi5-6.Maziwa ya mama hayana hayo madini ya kutosha,ni muhimu kutengeneza vyakula vyenye hayo madini chuma.
Kama mtoto wako ameanza kula vyakula,wataalam wengi wanashauri iron-fortified rice cereal ni chakula cha mwanzo kwa sababu ni aghalabu kuleta au sababisha allergy kama nafaka nyingine.Pindi mtoto anaendelea kukua,unaweza kuchanganya infant cereal na matunda.Ni vizuri ikawa laini au nyepesi na matunda kama pear, peach,na plum.
Cheese
Cheese ni nzuri yenye protein –ni muhimu kwa ukuaji-- na calcium kwa kujenga mifupa imara na meno. Cheese ina dose ya afya ya riboflavin (vitamin B2),ambayo husaidia kubadili protein, fat, na carbohydrates katika mfumo wa nguvu au energy. Swiss cheese kwa kawaida ni tamu na laini kwa watoto.Japo cheese huweza kuwa choking hazard,au kukatwa vipande pande. Ni nzuri kwa watoto wanaokula vitu vizima kama kidole na hutumika kwa vitu vingine pia .
kuku
kuku ana protein na ni chanzo cha vitamin B6,amabayo hutumika kusaidia kutia nguvu mwilini tokea kwenye vyakula.Ni muhimu kwa watoto kuanza kula mara kwa mara chakula chenye protein hata kwa uchache wake kusaidia ukuaji wa mtoto.Kama mtoto wako hapendi ladha ya kuku ile yenyewe,mchanganyie na matunda anayopenda au mboga anayoipenda.
Citrus fruits
Citrus fruits, ikiwemo chungwa, ndimu, na zabibu,ni nzuri na chanzo cha vitamin C,ambayo husaidia kutengeneza collagen inayopatikana kwenye mishipa ,mifupa,na tissues nyingine mwilini. Vitamin C pia huponesha palipoumia na kusaidia kuyeyuka kwa madini chuma kutokea kwenye vyakula vingine. Citrus fruits pia ina potassium, madini amabyo yanasiadia misuli kujikunja na kufanya kazi vizuri na kumaintain afya ya fluid balance mwilini.kuwa makini acid isizidi kwa mtoto,ni vizuri zaidi kutompa mtoto citrus fruits mpaka baada ya kutimiza au baada ya mwaka.
Nyama nyekundu(red meat)
Nyama nyekundu huleta kwa urahisi ya kuyeyusha aina ya madini chuma kwa mtoto wako.Madini chuma husaidia seli za damu nyekundu kubeba Oxygen kwenda kwenye seli kupitia mwilini na ni muhimu kwa kukuza akili au ubongo.Kwa bahati mbaya,upungufu wa madini chuma –ambayo huweza sababisha madhara katika usomaji na tabia pia-ni moja wapo ya upungufu wa lishe kawaida kwa watoto.
Ndio maana ni muhimu kuhakikisha mtoto wako anayapata haya madini chuma,kutokea kwenye nyama nyekundu,na vyanzo vingine katika mlo wake.Kwa watoto wadogo,weka nyama yenyewe haswa,kama beef na karoti.Watoto wakubwa ambao wanaweza kutafuna ipike vizuri kisha watumie hivyo.
Butternut Squash
Butternut squash ni nzuri kwa watoto sababu wanapenda ladha ya utamu.Ni chanzo kizuri cha antioxidant beta-carotene na pia ina vitamin C, potassium, fiber, folate, B-vitamins,na ina omega-3 fatty acids.Ni rahisi kutayarisha nyumbani kama utanunua ilo prepeeled, precut squash inayopatikana wanapotengeneza.Chemsha ichemke vizuri,kisha ikoroge mpaka ilainike.Tengeneza na uwaandalie kwa familia ni nzuri sana na ina ladha nzuri pia.
Samaki
Samaki weupe,kama vile haddock na cod,ni wazuri sana kwa protein,ambayo watoto wanaihitajia kwa maendeleo ya kukua. Samaki wa mafuta , kama salmon, huleta fat-soluble vitamins na mafuta yenyewe fats, kama DHA,ambayo inakuza akili na macho na kukuza mfumo wa immune. Samaki huweza sababisha allergy,kwahiyo ongea na mtaalam wa watoto kabla hujampatia mwanao.Kama iko POA,basi utamsababishia mtoto afya nzuri.Wataalam wanashauri ni vizuri kumlisha mtoto samaki mara mbili katika mlo wake kwa wiki yenye mercury kidogo,kwakuwa ina faida nyingi za kiafya kwa mtoto.
Nyanya
Nyanya ina lycopene nyingi, pigment nyekundu katika nyanya ina fanya kazi kama antioxidant kusaidia kulinda na cansa na vijidudu vya moyo. Lycopene huweza kuyeyeuka ikafanya kazi vizuri mwilini kama nyanya itakua imepikwa vizuri na mafuta.Kwahiyo tengeneza sauce ya tomato na tambi kwa kupika nyanya na mafuta ya olive oil.Saga iwe laini kwa watoto wanaoanza kula.Sauce ya kutengeneza nyumbani ina sukari,na chumvi kidogo kuliko ya kununua,na ni nzuri kwa familia yote.Hivi huna tomato fresh?basi hata za kwenye makopo ni nzuri pia.
Peas/Njegere
Peas huwa ina burst pamoja na vitamin K,lishe ambazo zinafanya kazi pamoja nazo ni calcium husaidia kujenga mifupa. Peas ni chanzo cha antioxidant vitamins A na C, na pia folic acid B vitamins. Na kumuwekea peas mtoto kwenye sahani yake ita boost fiber katika mlo wake,na ni muhimu sababu wataalam wameona watoto wote na hata na watoto wakubwa pia,hawapati fiber ya kutosha.Kusaga chakula cha watoto basi peas ni rahisi sana .
Broccoli
Broccoli ni kwakweli ni chakula kizuri ,ni chanzo kikuu cha vitamin C na pia ina beta-carotene, folic acid, madini chuma, potassium, na fiber.Kuchemsha broccoli katika maji hupunguza karibu nusu yake ya vitamin C ilokuwemo, kwahiyo ni vizuri kuisteam au kuweka kwenye microwave. Kama mwanao nimpenzi wa ladha ya broccoli,mchanganyie na kitu kitamu au mboga anayoipenda ,kama viazi vitamu au butternut squash.
Tambi(pasta)-makaroni
Tambi ina carbohydrates nyingi,ambayo huvunjwa vunjwa kusambaza guvu mwilini.Na ina ladha nzuri na ziko za shape nyingi tofauti tofauti zenye fun kibao,ambazo huvutia kwa watoto wa rika zote.Tambi nyingi zina vitamins na madini, kama folic acid,madini chuma, and B-vitamins. Ni mchanganyiko wa nafaka na ngano nzima ina fiber, lakini texture yake huweza kuwa nzito kwa mtoto .Tambi zenye shepu au umbo dogo dogo zipikwe vizuri hadi zilainike huwa ni chakula kizuri kwa watoto hata wakubwa kubwa pia mdogo.
WAZAZI: Chakula kizuri kwa mtoto/CHAKULA BORA KWA MTOTO MDOGO/ CHAKULA MAALUMU KWA WATOTO WA DODO/ MAMA NA MTOTO.