Friday, 15 June 2018
KABABU ZA NYAMA(MINCED MEAT KEBAB)
MAHITAJI
1.Nyama ya kusaga robo
1/4kg Minced Meat
2.Kitunguu maji kikubwa 1
1 Large size Onion
3.Vitunguu thomu punje kubwa 3
3 Garlic Cloves
4.Tangawizi kijiko Cha Chai1(ilotwanga)
1 Tea spoon minced Ginger
5.Pilipili ya kuwasha 1(au zaidi kama mpenzi wa pilipili)
1 Chilli Pepper or more
6.Ndimu 2
2 Lemon
7.Pilipili manga ya unga nusu kijiko cha chakula
1/2 Tbsp Black Pepper
8.Mdalasini wa unga nusu kijiko cha chakula
1/2 Tbsp Cinnamon powder
9.Uzile(Binzari nyembamba) ya unga Kijiko Cha Chakula 1
1 Tbsp Cumin powder
10.Mayai 3
3 Eggs
11.Chumvi kiasi
Salt to taste
12.Bread crumbs kikombe kidogo kimoja
1 small Cup Bread crumbs
13.Mafuta ya kupikia nusu lita
1/2 Litre of Cooking Oil
14.Pilipili hoho(Pilipili bogo) ndogo 1
1 Green pepper
15.Karoti ndogo 1(ilioparwa)
Grated carrots
16.Kebab Masala(sio lazima ila vizuri ukiwa navyo)
Kebab Masala (Optional)
MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Gawa nyama yako sehemu mbili sawa
Divide the minced meat into halves
2.Moja weka jikoni tia chumvi,ndimu usiweke maji acha itoe maji yenyewe hadi iwive
One half put it in the pan then add salt,lemon juice and bring it to boil till dry do not add water
3.Kisha changanya nyama mbichi na iloiva pamoja
Then mix the fresh minced meat and the cooked one into the bowl
4.Twanga kitunguu thomu,pilipili na chumvi na uviweke kwenye nyama
Grind garlic cloves,salt and chilli together and then add the mixture in the bowl of meat
5.Changanya nyama yako vizuri weka tangawizi,pilipili manga,mdalasini,uzile na uichanganye vizuri
Add the ginger,garlic mixture you grind before and the spices mentioned above into the meat and mix them well
6.Menya kitunguu maji,pilipili hoho vikate kate na viweka kwenye nyama
Peel the onion and green pepper then chop them into slice and add them into the meat mixture
7.Vunja yai moja weka kwenye nyama changanya vizuri mchanganyiko wako
Crack one egg add in the meat mixture and mix it well till mixed
8.Malizia kuweka Bread crumbs zako changanya mchanganyiko wako na onja chumvi kama haijakolea ongeza kidogo na uchanganye vizuri mchanganyiko wako.
Add the bread crumbs to the mixture and mix it well then taste if every thing is okay proceed next step
9.Weka Kebab masala kama unayo na uchanganye mchanganyiko wako
Add the kebab masala into the mixture and keep mixing till mixed
10.Chukua nyama yako tengeneza umbo la maduara madogo madogo mpaka umalize nyama yako.
Take a small portion of a mixture and shape it into several small balls
11.Andaa kibakuli kingine vunja mayai yako yalobakia weka na chumvi kidogo yachanganye na kijiko au umma na yaweke pembeni
Break two eggs remained in a separate bowl,add pinch of salt then beat them with spoon or folk
JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Weka mafuta kwenye karai yaache yapate moto sana
Heat the oil in a pan to a maximum
2.Chukua maduara yako yachovye kwenye mayai kisha dumbukiza kwenye mafuta
Soak the round balls into the beaten egg and add into the heated oil
3.Ziache dakika 3 kisha zigeuze na ziwache kidogo
Leave for 3 minutes and turn into other side
4.Zikiwa za brown zitoe weka kwenye chujio au tissue zichuje mafuta
When they turn into golden brown remove them and take into sieve or tissue
5.Weka kwenye sahani inapendeza uweke na chatne wakati wa kula
When they get dried serve with chatne
6.Unaweza kula kababu zako na Chapati au mkate wowote ule.
You can serve with bread,chapati,juice or as they are.
Angalizo/Note:
1.Ili kababu zipendeze hakikisha zinachapuka viungo vizuri
Marinate the mixture well so as kababu may have good taste
2.Mayai ya kuchovyea wakati wa kupikia yawe ya kutosha
Beat the enough egg for soaking the kababu
3.Mafuta yasipopata moto vizuri kababu zinaweza kupasuka kwenye mafuta
If you hurry to add the kebabu before the oil get heated well the kebab will break during frying
4.Zipike taratibu usizifanyie haraka ili ziive ndani vizuri
Make sure you don't flip or remove the kababu until they turn into golden color otherwise the inner side will be uncooked
5.Usizifanyie haraka kuzigeuza hakikisha zinapiga rangi ya brown ndio uzigeuze
Don't flip to the other side if they do not turn into golden brown
Furahia Kababu Zako
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...
-
Futari ya Mihogo na Viaz Vitamu Kila kitu unapokifanya kwa mfululizo kwa muda mrefu kinachosha. Hata kupika nako kunachosha,i...
-
MAHITAJI/INGREDIENTS Visheti 1.Unga wa Ngano ¼ Kg ¼ Kg Plain Purpose Flour 2.Maziwa ya maji Kikombe Kidogo 1 1 Small Cup...
-
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...
No comments:
Post a Comment