Thursday, 14 June 2018

SUPU YA SAMAKI



MAHITAJI/INGREDIENTS
1. Samaki Vipande 3
 3 Pieces of Fish

2. Keroti ndogo 1
 1 Carrot

3. Pilipili Hoho(Pilipili boga) 1
 1 Green Pepper

4. Viazi Mbatata 3
 3 Potatoes

5. Kitunguu thomu Punje 2
 2 Cloves Garlic

6. Ndimu 1
 1 Lemon

7. Tangawizi ilotwangwa kijiko kidogo 1
 1 Tbsp grinded Ginger

8. Maji Lita 1
 1 Litre of Water

9. Pilipili Mbuzi 2
 2 Red Chilli

10. Royco/Fish Masala/Curry Powder kijiko 1
 1 Tbsp Royco/Fish Masala/Curry Powder

11. Chumvi kijiko Kikubwa 1 ½
 1 1/2 Tbsp of Salt


MAANDALIZI/PREPARATION


Osha Samaki Vizuri weka kando
Wash well those 3 pieces of fish
Menya Viazi Mbatata
Peel the Potatoes
Osha viungo Vyako Vilobakia
Wash all remaining ingredients

Katakata keroti,pilipili boga weka pembeni
Cut carrots and green pepper into different pieces and size as you pleased

Twanga kitunguu Thomu
Mince the garlic cloves
JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK


Weka samaki kwenye sufuria ya kupikia
Place the fish into cooking bowl
Kata sehemu mbili sawa viazi mbatata na viweke kwenye sufuria
Cut the potatoes each into half
Weka Keroti,Pilipili boga
Add the pieces of carrots ,green pepper
Kisha malizia kuweka vitu vyote vilotajwa hapo juu kasoro ndimu,pilipili na royco au masala yoyote ulionayo
Then add all ingredients mentioned above except lemon and masala
Weka jikoni acha ichemke,samaki akianza kuiva weka royco au masala yoyote ulionayo
Put your cooking bowl on stove let it boil till the fish is starting to get boiled then add any kind of masala
Koroga kisha kamua ndimu weka
Steer your soup then add a juice of lemon
Acha kwa dakika 2 weka pilipili zako usizipasue funika supu kwa dakika 1 ipate harufu ya pilipili
Leave it for 2 minute then add red chill as it is without cut it into pieces then cover it so as the soup to have nice smell of chilli
Funua angalia kama kila kitu kimeiva onja halafu epua
Uncover it and test the soup if everything is Ok
Weka kwenye Mabakuli tayari kwa kuliwa na Chapati au mkate uupendao
Pour your soup into bowl and serve it

Angalizo:Note
1. Hakikisha unaonja chumvi kama imepungua uweze kuongeza
   Make sure you taste the salt and add it if needed
2. Kuwa makini samaki au viazi visivurugike kwa kuvichemsha sana
    Dont over boil the soup
3. Weka pilipili nzima ili hata asiependa pilipili aweze kula supu yako
    Dont cut the red Chilli so as any one can eat your soup
4. Usiweke ndimu mapema husababisha supu iwe chungu
    Dont put lemon juice earlier
5. Supu hii ni kwa ajili ya watu watatu
  This soup is for three people
 
Furahia Supu Yako.
Enjoy Your Soup

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...