Thursday, 7 June 2018

Mapishi ya makande ya nazi na karanga




Mahitaji

  • Mahindi yaliyokobolewa – kilo 1½
  • Maharage ½ kilo
  • Vitunguu maji 3
  • Nyanya 2
  • Karanga ¼ kilo
  • Njugu mawe ½ kilo 
  • Pilipili hoho 1
  • Chumvi kijiko 1 cha chai
  • Mafuta ¼ lita
  • Nazi kubwa 2.
  •  
  •  
  •  

    Maelekezo

  • Chambua maharage, mahindi, karanga nanjugu mawe kisha osha vizuri.
  • Changanya maharage, mahindi na njungumawe pamoja.
  • Bandika sufuria ya maji jikoni. Weka mchanganyiko wa maharage, weka chumvi kisha acha mchanganyiko uchemke vizuri. Kwa kawaida maharage yanachukua muda mrefu kuiva vizuri. Hivyo unaweza kusubiria takribani dakika 25-30 ili kuhakikisha yameiva. Kama maji yakikauka kabla ya maharage kuiva, ongeza maji kiasi ili yaive vizuri.
  • Andaa vitunguu, pilipili hoho na nyanya kwa kuosha kisha kuvikata vipande vidogo vidogo. Weka vizuri na kusubiria kuvichanganya na makande.
  • Andaa tui la nazi kwa kuchuja tui zito ili liwe tayari kuchanganya na chakula.
  • Kama maharage na njugu mawe yakikaribia kuiva (takribani dakika 30) weka karanga kwenye mchanganyiko. Koroga ili vichanganyike vizuri. Acha iendelee kuchemka na subiria hadi mchanganyiko uive vizuri. Mchanganyiko ukiiva vizuri toa jikoni na hifadhi pembeni.
  • Bandika sufuria, weka mafuta ya kula kisha acha yachemke.
  • Mafuta yakipata moto vizuri weka vitunguu kisha koroga koroga hadi vibadilike rangi na kuanza kuwa na rangi ya udongo.
  • Weka pilipili hoho, karoti. Koroga kiasi kwa muda wa dakika 2 hadi 3.
  • Weka nyanya, koroga kiasi na kisha funika na mfuniko. Acha nyanya ziive vizuri kwa mvuke ili ziwe laini. Baada ya dakika 6-8 unaweza kuponda ua kusaga nyanya ili kupata mchuzi wenye rojo. Koroga ili kupata mchanganyiko mzuri.
  • Nyanya zikiiva vizuri weka mchanganyiko wa maharage kwenye sufuria. Koroga vizuri hadi mchangyiko uwe sawia. Onja ili kujua kama kiwango cha chumvi kinatosha. Unaweza kuongeza kama haitoshi.
  • Weka tui la nazi huku ukikoroga ili kuzuia tui kukatika. Koroga hadi ianze kuchemka.
  • Funika sufuria na subiria kwa muda wa dakika 10, kisha ipua chakula jikoni ili upate kujiramba.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...