Mahitaji
- Nyama ya kusaga kilo 1
- Vitunguu maji 2
- Vitunguu saumu 2
- Tangawizi 1
- Nyanya 4
- Mafuta ¼ lita
- Chumvi kijiko 1 cha chai
- Karoti 2
- Pilipili hoho 1
- Ndimu. 1
Maelekezo
- Menya vitunguu na ukate kwenye vipande vyembamba sana
- Menya na kwangua karoti iwe kama uji
- Menya pilipili hoho na kisha kata vipande vyembamba
- Menya nyanya na zikate kawaida
- Menya, osha na kisha kwangua tangawizi
- Twanga vitunguu saumu
- Bandika sufuria ya kupikia jikoni
- Weka nyama na anza kukoroga ili kuzuia isigandie kwenye sufuria na kuungua
- Weka kitunguu maji huku ukiendelea kukoroga kwa muda wa dakika 10
- Weka kitunguu saumu na tangawiizi. Endela kukoroga kwa muda wa dakika 5 zaidi.
- Weka mafuta kidogo sana ili kufanya viungo viize.
- Weka pilipili hoho, karoti na kamulia ndimu. Ongeza chumvi kidogo. Endelea kukoroga.
- Weka nyanya, koroga na funika sufuria na mfuniko kwa muda kama dakika 10.
- Funua angalia kama imeiva. Unaweza kujiramba.
No comments:
Post a Comment