Mahitaji
- Ndizi mbichi 6
- Nazi 1
- Vitunguu 2
- Pilipili hoho 1
- Karoti 2
- Nyanya 3
- Chumvi kijiko 1 kikubwa
Maelekezo
- Menya ndizi kisha ziweke kwenye maji. Hii inasaidia kutopata weusi na utomvu unaotokana na kutokuwa kwenye maji. Kisha osha ndizi zako na uweke tena kwenye chombo chenye maji mengi.
- Menya vitunguu na kisha katakata vipande vidogo.
- Kata pilipili hoho, menya nyanya uzikate vipande.
- Kata karoti na nyingine kwangua maganda.
- Andaa nazi kwa kuikuna na kukamua tui 2 – moja tui zito weka kwenye chombo pembeni na tui jepesi kwenye chombo tofauti.
- Bandika chungu au sufuria ya kupikia jikoni. Ongeza tui zito kidogo, acha lichemke mpaka litoe mafuta.
- Tui likishatoa mafuta, weka vitunguu vyako mpaka vikaribie kuiva halafu ongeza pilipili hoho. Koroga kiasi halafu weka karoti. Endelea kukoroga mchanganyiko kwa dakika 2 halafu ongeza nyanya kwenye sufuria. Ongeza chumvi na kisha funika sufuria na mfuniko hadi nyanya ziive (takribani dakika 5 hadi 8).
- Nyanya zikiiva, ongeza ndizi kwenye sufuria yenye viungo. Endelea kukoroga.
- Ongeza tui jepesi kwenye sufuria yenye ndizi huku unaendelea koroga ili tui lisikatike.
- Ikishachemka, ongeza na kupungua tui, ongeza tui zito huku ukiendelea koroga mpaka lichemke.
- Acha mchanganyiko uchemke kwa takribani dakika 10 ili tui liive.
- Ndizi zako zitakua zimeiva.
No comments:
Post a Comment