Supu Ya Kuku Na Viazi/Mbatata
VIPIMO :
Kuku 4 LB
Viazi/mbatata 3
Kitunguu maji 1
Kitunguu thomu 5 chembe
Pilipili mbichi 2
Nyanya ya kusaga 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga ½ kijiko cha chai
Haldi/tumeric/bizari ya manjano ¼ kijiko cha chai
Mafuta ya zaytuni 2 vijiko vya supu
Kotmiri (coriander freshi) 1 msongo
Ndimu/siki 2 vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Kuku 4 LB
Viazi/mbatata 3
Kitunguu maji 1
Kitunguu thomu 5 chembe
Pilipili mbichi 2
Nyanya ya kusaga 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga ½ kijiko cha chai
Haldi/tumeric/bizari ya manjano ¼ kijiko cha chai
Mafuta ya zaytuni 2 vijiko vya supu
Kotmiri (coriander freshi) 1 msongo
Ndimu/siki 2 vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha kuku na ukate vipande vipande kiasi
- Menya viazi/mbatata, katakata vipande kiasi.
- Menya kitunguu maji ukate vidogodogo
- Weka mafuta katika sufuria, kisha tia vitunguu vikaange kidogo tu hadi viwe laini.
- Kisha tia vipande vya kuku, chumvi, pilipili manga, thomu ilochunwa (grated) au kukatwakatwa vipande vidogodogo.
- Tia nyanya, haldi, na maji kiasi.
- Tia viazi/mbatata na iache ichemke hadi kuku na viazi/mbatata ziive.
- Katakata kotmiri na pilipili mbichi ndogo ndogo utie mwishoni.
- Tia ndimu au siki ikiwa tayari kuliwa na mkate au upendavyo
No comments:
Post a Comment