Viazi Vyekundu Vya Masala
VIPIMO :
Viazi /mbatata 10 kiasi
Kitunguu maji kilichosagwa 1
Thomu iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Pilipili iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Rai (mustard seeds) 1 kijiko cha supu
Majani ya mchuzi (curry leaves) 7 majani
Uwatu uliosagwa (methi) 1 kijiko cha chai
Nyanya kopo 5 vijiko vya supu
Ndimu 3 vijiko vya supu
Mafuta ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Viazi /mbatata 10 kiasi
Kitunguu maji kilichosagwa 1
Thomu iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Pilipili iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Rai (mustard seeds) 1 kijiko cha supu
Majani ya mchuzi (curry leaves) 7 majani
Uwatu uliosagwa (methi) 1 kijiko cha chai
Nyanya kopo 5 vijiko vya supu
Ndimu 3 vijiko vya supu
Mafuta ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Chemsha viazi kiasi viwive lakini visivurugike
- Menya, katakata vipande weka kando.
- Tia mafuta katika sufuria, yakishika moto tia rai, zikaange kwa muda wa dakika moja hadi zigeuke rangi kidogo.
- Tia majani ya mchuzi, uwatu, thomu, kitunguu maji, pilipili kaanga kidogo tena.
- Tia nyanya kopo endelea kukaanga kidogo kisha tia chumvi, ndimu na maji kiasi kidogo ili kufanya rojo kiasi.
- Mimina viazi, changanya, pakua katika sahani.
No comments:
Post a Comment