Kuku wa giligilani na chovyo ya Asali
Kuku wa giligilani na chovyo ya Asali
Mahitaji
- Kuku kilo 1,chemsha na chumvi na kitunguu swaumu.
- Unga wa ngano vijiko 6 vya chakula
- Myai matatu
- Giligiliani Vijiko 2 vya chai.ponda view laini sana
- Vitunguu maji vijiko 3 vya chakula,kata vipande vidogo sana
- Pilipili manga ½ kijiko cha chai
- Maji robo kikombe (tumia kwa awamu)
Mbili:Chovyo
- Asali ½ kikombe
- Tangawizi ya unga vijiko 3 vya chai
- Apple cidr vinegar vijiko 3 vya chakula
1. chemsha kuku aive na maji yote yakauke,acha apoe
2.katika bakuli kubwa weka mahitaji yote ya namba moja,changanya adi upate uji mzito na laini.
3.Bandika mafuta jikoni yapate moto,yasiwe yamoto sana
- Mafuta yakiwa yamoto sana nyama itaungua kabla haijaiva
- Mafuta yakiwa yamoto sana ukiweka kuku mafuta huruka na yanaweza kukuunguza
- Mafuta yakiwa yamoto sana yanafanya kuku ajae hewa na kisha kupasuka na kurusha mafuta
5.Toa kwenye mafuta weka kwenye chujio la mafuta ili kudondoshe mafuta,kisha hamisha na weka kwenye sahani iliyotandikwa karatasi safi yajikoni ili kutoa mafuta yaliyobaki.Kuku tayari
Kuandaa Chovyo
1.katika bakuli,weka mahitaji yote ya namba mbili,changanya vizuri ili kupata rojo .Chovyo tayari
Weka kuku katika sahani na chovyo katika bakuli kisha tenga kwa pamoja. Chovya kipande chakuku kwenye chovyo kisha kula.Unaweza kula na chakula chochote upendacho.hapa jikoni tulikula na karoti zakuchemsha.
No comments:
Post a Comment