Sunday, 30 September 2018
Roast ya nyama iliyoungwa na karanga
Nilidoea mapishi haya kwa jirani, nikapagawa na nikalazimika kuyapika kwangu siku inayofuatia. Si mapishi magumu, bali ni tofauti na yale niliyozoea kuandaa kwangu hakika yamenipa raha. Ni aina ya mapishi yamezoeleka sana Afrika magharibi – najua wotu tunaunga kwa karanga, ila upishi wake niliupenda. Najua ukijaribu utayapenda, jirambe na utamu huu. Usikose kuelezea utamu uliopata ukishajiramba.
Kuandaa: dakika 15
Mapishi: dakika 30
Mahitaji
Nyama - 1/2 kilo
Karanga zilizosagwa/ peanut butter - vijiko 3 vikubwa
Mafuta ya kula - 1/4 lita
Chumvi
Tangawizi - 1
Kitunguu saumu - 1
Kitunguu maji - 2
Nyanya - 4
Nyanya chungu - 4
Cube magic
Viazi - 6
Viungo vingine upendavyo kwenye sauce*.
Maelekezo
Mapishi na Isatou Keita
Tayarisha nyama - kata, osha, weka chumvi, tangawizi na kitunguu saumu. Acha ikae kwa dakika 45 hadi saa 1 ili viungo viingie vizuri.
Bandika sufuria jikoni, weka mafuta kiasi. Subiria yapate moto.
Weka nyama kwenye mafuta. Fanya kama unaikaanga - koroga ili ichanganyike vizuri na mafuta. Funika sufuria au chungu na mfuniko ili nyama ijipike kwa mvuke wake vizuri.
Geuza geuza nyama kila mara ili kuzuia isigande kwenye chombo cha kupikia. Subiria hadi iive.
Unaweza kubadilisha sufuria maana utakayokaangia nyama itakuwa na mafuta yenye masalia ya viungo. Badilisha sufuria kwa kumimina mafuta kwenye sufuria nyingine, acha ipate moto - weka mafuta na kisha weka nyama yako ili uendelee na mapishi.
Weka vitunguu kwenye nyama, koroga hadi viive.
Weka nyanya, koroga kisha funika. Subirie zipate kuiva.
Ongeza karoti, pilipili hoho, na viambato vingine utakavyo.
Anza kuandaa peanut butter (au karanga za kusaga) kwa kuweka vijiko 3 ya vikubwa kwenye bakuli ya plastiki.
Ongeza maji ya uvuguvugu kiasi, na uanze kusaga, kukoroga au kufinyanga kwa mkono ili karanga zichanganyike vizuri na maji kuwa kama uji mzito. Ni vizuri ukipata rojorojo nzuri maana itakuwa rahisi kuchanganyika na mchuzi.
Ukishapata mchanganyio mzuri, weka karanga kwenye chungu cha nyama jikoni. Koroga hadi mchanganyiko uwe vizuri. Ongeza maji kama robo kikombe ili upate kulainisha rojo. Funika chungu chako.
Menya, osha na kata viazi mviringo vyako kwenye vipande vidogo na hifadhi kwenye maji.
Menya osha na kata nyanya chungu - au unaweza kuweka zikiwa nzima nzima.
Mchanganyiko ukishachemka, Weka viazi na nyanya chungu. Subiria mchanganyiko uchemke, halafu weka cube maggi. Koroga ili kuifanya ichanganyike vizuri na mboga.
Unaweza kuongeza tui la nazi au maziwa kuongeza ladha ya mboga.
Subiria dakika 4 hadi 5 baada ya kuongeza cube maggie kisha ongeza pilipili manga ya kusaga. Weka pilipili manga mwisho sababu ikiwa hupoteza ladha kirahisi kwenye moto mkali.
Viazi vikishaiva, unaweza kutenga mboga yako na chakula ujirambe.
Unaweza kula mboga hii vitu tofauti mfano wali, mkate, ugali, maandazi, tambi, mihogo, viazi, chapati au chochote kile kukupa ladha uipendayo.
Usisahau kutupa matokeo ya mapishi yako. Na usiache kushare na wenzio, maana mapishi matamu huwa tunawaambia wale tunaowajali
Jali uwapendao, wape uhondo wa misosi wajirambe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...
-
Futari ya Mihogo na Viaz Vitamu Kila kitu unapokifanya kwa mfululizo kwa muda mrefu kinachosha. Hata kupika nako kunachosha,i...
-
MAHITAJI/INGREDIENTS Visheti 1.Unga wa Ngano ¼ Kg ¼ Kg Plain Purpose Flour 2.Maziwa ya maji Kikombe Kidogo 1 1 Small Cup...
-
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...
No comments:
Post a Comment