Mahitaji
- 240 gram mchele wa Basmati
- 120 gram njegele za kumenywa (chickpeas)
- 3 majani ya kitunguu maji (spring onions), kata kata
- 1 fungu la giligilani chop chop
- 1 fungu la parsley chop chop
- 1 kijiko kikubwa cha cakula siagi (butter) kwakuongeza ladha ya chakula
- Chumvi kulingana na ladha upendayo
Jinsi ya kupika
- Chukua kikaango weka siagi ikisha ikiyeyuka weka majani kiasi ya kitunguu maji na uendelee kukaanga. Kisha chuja mchelewako wa basmati nao weka ukiwa mkavu na endelea kukaanga mpaka unukie.
- Weka chumvi pamoja na njegere koroga kiasi.
- Kisha weka maji safi 400 ml (hii inategemea na kiwango cha mchele wako) kisha funika mfuniko wa kikaango au sufuria yako na pika kwa dakika 10.
- Weka chop parsley na chop giligilani kisha koroga zichanganyike na wali wako.
- Baada ya hapo wali wako utakua umeiva na unaweza kula na mboga yoyote upendayo.
No comments:
Post a Comment