Tuesday, 2 October 2018
JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA BUNS ZA SUKARI NYUMBANI
Vipimo
Unga - 3 Vikombe vya chai
Maziwa - 1 Kikombe cha chai
Sukari - ¼ Kikombe cha chai
Siagi - ¼ Kikombe cha chai
Chumvi - ½ Kijiko cha supu
Yai - 1
Hamira - 2 ¼ Vijiko vya chai (pakiti 1)
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Katika kibakuli changanya sukari na ½ kikombe ya maziwa yaliyo vuguvugu, kisha tia hamira, koroga na iwache dakika 5 hivi.
Halafu tia yai na yale maziwa ½ kikombe yaliyobakia na siagi iliyoyeyushwa.
Katika bakuli jengine, changanya unga na chumvi kisha ongezea ule mchanganyiko wa hamira.
Kisha ukande unga baada ya kuinyunyizia unga ili usishike.
Ukipenda unaulaza unga firijini kuongeza ladha au unafanya viduara kama 16 na kuziweka kwenye trei ya kuchomea iliyopakwa siagi.
Ziache pahali penye joto hadi ziemuuke.
Washa oveni moto wa 350ยบ.
Piga yai na kijiko kimoja cha maziwa, kisha pakiza juu kabla hujachoma.
Vumbika kwenye oveni kwa muda wa dakika 15 au mpaka zibadilike rangi na viweke kwenye sahani na tayari kwa kuliwa. Asante
JINSI YA KUANADAA NA KUPIKA PILAU YA NYAMA NYUMBANI.
Vipimo
Mpunga - 4 vikombe
Nyama - 1 kilo moja
Kitunguu maji - 3
Mbatata/viazi - 7 vidogodogo
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa 3 vijiko cha supu
Bizari nzima/ya pilau/uzile/cumin - 3 vijiko vya supu
Mdalasini - 3 vipande
Hiliki - 7 punje
Pilipili manga nzima - 1 kijiko cha supu
Chumvi kiasi
Mafuta - ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele weka kando
Katakataka vitunguu slice ndogo ndogo.
Weka mafuta katika sufuria kisha ukaange vitunguu pamoja na mdalasini, hiliki pilipilimanga.
Vitunguu vikigeuka rangi unatia kitunguu thomu na tangawizi.
Tia supu kidogo na nyama, kisha tia bizari ya pilau/uzile, na viazi/mbatata.
Maliza kutia supu yote, na ikiwa ni kidogo ongeze maji kiasi cha kuivisha mchele. kisha tia mchele ufunike hadi wali uwe tayari.
Ikiwa unatumia mkaa palia juu yake, ikiwa hutumii uache uive kwa moto mdogo mdogo.
TAG RAFIKI YAKO AJE KUJIFUNZA HAPA
JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA BAGIA ZA DENGU NA VIAZI NYUMBANI.
Vipimo
Unga wa dengu - 3 vikombe vikubwa
Chumvi - 1 kijiko cha chai
Mbatata (kiazi) - 1
Maji baridi - 1 glass
Baking powder - 1 cha chai
Kotmiri iliyokatwakatwa - 4 -5 Miche
Kitunguu maji kilosagwa - 2 kijiko cha supu
Kitunguu saumu(thomu) ilosagwa au ya unga - 1 kijiko cha chai
Mafuta - 500 ml
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Tumia bakuli lenye nafasi mimina unga na viungo vyote.
Tia maji ukitumia uma au mchapo wa mkono (usotumia umeme) kuvuruga mchanganyo.
Ukisha kuwa laini bila mavimbo, hakikisha si mzito na si uji sana (mwembamba). Menya kiazi na kwaruza kiwe mithili ya tambi kisha tia ndani ya unga vuruga uchanganyike.
Uwache kwa muda wa robo saa (dakika 15) paka 20.
Weka karai jikoni au sufuria nzito ndogo, tia mafuta na acha yapate moto sawasawa.
Tumia kijiko cha supu kuteka unga kutia kwenye mafuta , unapotia hakikisha kipimo chako chote kimelenga mahala au sehemu moja bila ya kutapakaza ili uweze kupata kidonge .
Utaenedelea hivi kwa kujaza karai nafasi yote zikigeuka rangi ya kuiva, unazigeuza upande wa pili paka umalize zikiwiva kwa rangi nzuri.
Tumia sahani ukiwa umetandaza karatasi za jikoni kuweza kuchuja mafuta baada ya kuchoma. Kisha badilisha kwenye sahani au bakuli nyengine, tayari kuliwa
Kidokezo:
Huliwa kwa chatini ya aina yoyote, na unapochoma ukiona unga haupandi juu basi lazima kuna itilafu.
#mapishi #mapishigram #mapishiyetu
Sunday, 30 September 2018
Roast ya nyama iliyoungwa na karanga
Nilidoea mapishi haya kwa jirani, nikapagawa na nikalazimika kuyapika kwangu siku inayofuatia. Si mapishi magumu, bali ni tofauti na yale niliyozoea kuandaa kwangu hakika yamenipa raha. Ni aina ya mapishi yamezoeleka sana Afrika magharibi – najua wotu tunaunga kwa karanga, ila upishi wake niliupenda. Najua ukijaribu utayapenda, jirambe na utamu huu. Usikose kuelezea utamu uliopata ukishajiramba.
Kuandaa: dakika 15
Mapishi: dakika 30
Mahitaji
Nyama - 1/2 kilo
Karanga zilizosagwa/ peanut butter - vijiko 3 vikubwa
Mafuta ya kula - 1/4 lita
Chumvi
Tangawizi - 1
Kitunguu saumu - 1
Kitunguu maji - 2
Nyanya - 4
Nyanya chungu - 4
Cube magic
Viazi - 6
Viungo vingine upendavyo kwenye sauce*.
Maelekezo
Mapishi na Isatou Keita
Tayarisha nyama - kata, osha, weka chumvi, tangawizi na kitunguu saumu. Acha ikae kwa dakika 45 hadi saa 1 ili viungo viingie vizuri.
Bandika sufuria jikoni, weka mafuta kiasi. Subiria yapate moto.
Weka nyama kwenye mafuta. Fanya kama unaikaanga - koroga ili ichanganyike vizuri na mafuta. Funika sufuria au chungu na mfuniko ili nyama ijipike kwa mvuke wake vizuri.
Geuza geuza nyama kila mara ili kuzuia isigande kwenye chombo cha kupikia. Subiria hadi iive.
Unaweza kubadilisha sufuria maana utakayokaangia nyama itakuwa na mafuta yenye masalia ya viungo. Badilisha sufuria kwa kumimina mafuta kwenye sufuria nyingine, acha ipate moto - weka mafuta na kisha weka nyama yako ili uendelee na mapishi.
Weka vitunguu kwenye nyama, koroga hadi viive.
Weka nyanya, koroga kisha funika. Subirie zipate kuiva.
Ongeza karoti, pilipili hoho, na viambato vingine utakavyo.
Anza kuandaa peanut butter (au karanga za kusaga) kwa kuweka vijiko 3 ya vikubwa kwenye bakuli ya plastiki.
Ongeza maji ya uvuguvugu kiasi, na uanze kusaga, kukoroga au kufinyanga kwa mkono ili karanga zichanganyike vizuri na maji kuwa kama uji mzito. Ni vizuri ukipata rojorojo nzuri maana itakuwa rahisi kuchanganyika na mchuzi.
Ukishapata mchanganyio mzuri, weka karanga kwenye chungu cha nyama jikoni. Koroga hadi mchanganyiko uwe vizuri. Ongeza maji kama robo kikombe ili upate kulainisha rojo. Funika chungu chako.
Menya, osha na kata viazi mviringo vyako kwenye vipande vidogo na hifadhi kwenye maji.
Menya osha na kata nyanya chungu - au unaweza kuweka zikiwa nzima nzima.
Mchanganyiko ukishachemka, Weka viazi na nyanya chungu. Subiria mchanganyiko uchemke, halafu weka cube maggi. Koroga ili kuifanya ichanganyike vizuri na mboga.
Unaweza kuongeza tui la nazi au maziwa kuongeza ladha ya mboga.
Subiria dakika 4 hadi 5 baada ya kuongeza cube maggie kisha ongeza pilipili manga ya kusaga. Weka pilipili manga mwisho sababu ikiwa hupoteza ladha kirahisi kwenye moto mkali.
Viazi vikishaiva, unaweza kutenga mboga yako na chakula ujirambe.
Unaweza kula mboga hii vitu tofauti mfano wali, mkate, ugali, maandazi, tambi, mihogo, viazi, chapati au chochote kile kukupa ladha uipendayo.
Usisahau kutupa matokeo ya mapishi yako. Na usiache kushare na wenzio, maana mapishi matamu huwa tunawaambia wale tunaowajali
Jali uwapendao, wape uhondo wa misosi wajirambe
JIFUNZE KUPIKA SWAHILI: Chips na kuku
Chips zilizochanganywa na kuku, chakula hiki ni kizuri na rahisi kuandaa. Radha ya chakula hiki ni nzuri sana na utafurahia.
Kuandaa: dakika 15
Mapishi: dakika 45
Mahitaji
Kuku ½ kg
Viazi ulaya ½ kilo
Nyanya 2 kubwa zilizoiva vizuri
Kitunguu saumu ¼ kijiko cha chai
Tangawizi ¼ kijiko cha chai
Korianda ¼ kijiko cha chai
Hing ¼ kijiko cha chai
Chumvi ½ kijiko cha chai
Pilipili manga kijiko 1 cha chai
Mafuta ya kula
Apple cider vinegar ½ kikombe cha kahawa
Oyster sauce vijiko 2 vya chakula
Kitunguu maji 1
Maelekezo
Menya viazi kisha kata ukubwa wa chips unaopenda. Hifadhi vizuri kwenye maji yaliyowekwa chumvi.
Safisha kuku vizuri kisha weka kwenye sufuria safi. Mwagia vinegar juu ya kuku. Bandika sufuria ya kuku jikoni. Acha ichemke vizuri. Kisha toa na hifadhi pembeni.
Bandika kikaango, weka mafuta ya kula. Mafuta yakipata moto weka viazi na kaanga hadi chips ziive. Epua na hifadhi pembeni. Rudia hadi viazi vyote viwe vimepikwa.
Kaanga kuku kwenye mafuta uliyotumia kupikia chips.
Bandika sufuria jikoni, weka mafuta. Yakipata moto weka kitungu maji na viungo vyote ila usiweke nyanya na oyster sauce. Vitunguu vikianza kubadilika rangi weka nyanya. Nyanya zikiwa tayari weka kuku na funika vizuri kwa dakika 5 kisha weka oyster sauce. Ongeza supu ya kuku nusu kikombe kwenye sufuria, acha ichemke.
Weka chips kwenye sufuria lenye sauce ya kuku, pika hadi supu ikaukie.
Epua, tenga chakula na jirambe.
Pizza yenye topping ya kuku na cheese
Pizza, chakula rahisi kuandaa unachoweza kula wakati wowote - asubuhi, mchana au usiku. Ni vizuri kuandaa siku unayotaka kula chakula na kupumzika vizuri ukiwa unaongea na familia, marafiki au wengine Ni chakula chepesi, chenye virutubisho vingi na pia ni kitamu sana. Unaweza kuongeza vitu unavyopenda kuipendezesha pizza yako. Mapishi haya yameandaliwa na nnjosie, asante kwa kutushirikisha kwenye kujiramba na utamu wa misosi.
Kuandaa: dakika 75
Mapishi: dakika 35
Mahitaji
Kwa ajili ya unga:
Vijiko 2 vya chai vya hamira (yeast)
Vikombe 1 ¾ vya unga wa ngano. Tenganisha, weka kidogo pembeni
¾ ya kikombe cha maji ya uvuguvugu
Chumvi kijiko 1 cha chai
½ kijiko cha mafuta ya Olive (Mafuta ya mizeituni)
Kwa ajili ya topping:
Minofu ya kuku
Mixed herbs vijiko 2 vya chakula
Nyanya 2 kubwa
Pilipili hoho 1 na nusu
Mozzarella cheese
Kitunguu saumu vijiko 3 vya chakula vilivyosagwa
Butter vijiko 2 vya chakula
Pilipili manga kijiko 1 cha chai
Mapishi haya ya pizza unayoweza kuandaa kirahisi nyumbani yameandaliwa na nnjosie. Kwa ujumla pizza hii imeandaliwa kwa kufuata maelezo kama ilivyoandikwa hapa, lakini imetumia topping ya kuku, butter, mozarella na pilipili manga.
Andaa pizza kama ilivyoezwa hapa.
Pasha oven nyuzi joto 350°F (180°C). Bandika minofu ya kuku jikoni, acha ichemke kwa dakika 15. Weka pembeni ipoe.
Kwenye kikango, weka butter acha iyeyuke, kisha weka kitunguu saumu kijiko 1, mixed herbs na pilipili manga. Epua acha ipoe weka kwenye friji kwa muda.
Sambaza butter iliyotoka kwenye friji juu ya pizza kwa tumia kijiko. Weka kuku, nyanya, pilipili hoho kisha nyunyizia kitunguu saumu. Weka mozzarella cheese na nyunyizia mixed herbs. Oka Pizza kwa dakika 15 mpaka 20.
Epua. Jirambe.
Keki ya chocolate, maziwa na ndizi
Utamu wa hii cake ni zaidi ya maelezo. Uwepo wa chocolate unaifanya ivutie kwa macho, vanilla inaipa harufu tamu na utamu wake ni zaidi ya muonekano. Ni kitafunwa vizuri wakati wowote ili kuipa familia ladha tamu na mabadiliko.
Kuandaa: dakika 15
Mapishi: dakika 60
Walaji: 8
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Mahitaji
Unga wa ngano vikombe 2
Sukari kikombe 1
Ndizi 2, zilizoiva vizuri
Mayai 2
Mafuta ya kula ½ kikombe (Au butter 2/3 kikombe)
Chumvi kijiko 1 kidogo
Kikombe 1½ cha maziwa
Baking soda kijiko 1 kidogo
½ kikombe cha cocoa ya kuokea (Au chocolate ya unga)
Vanilla flavor kijiko 1 kikubwa
Hii ni keki unayoandaa ukiwa na muda na hamu ya kula kitu kitamu, chenye afya na kinachoweza kukupa furaha. Ni muhimu kuandaa keki kama una muda mwingi wakati wa weekend, ili upate matokeo mazuri zaidi na kujumuika vizuri na familia.
Washa oven weka kwenye nyuzi 350°F (180°C). Acha ipate moto.
Kwenye bakuli kubwa, changanya butter na sukari hadi zichanganyike na kuwa laini. Ongeza mayai, moja baada ya jingine – pasua kisha changanya vizuri.
Kwenye chombo tofauti, changanya unga wa ngano, cocoa, vanilla flavor, baking soda na chumvi. Koroga vizuri. Changanya mchanganyiko huu kwenye bakuli lenye mchanganyiko wa mafuta na sukari. Kwenye chombo tofauti, ponda ndizi hadi zilainike vizuri kisha weka kwenye mchanganyiko wa unga na mafuta. Koroga vizuri.
Ongeza maziwa kidogo kwa wamu kwenye mchanganyiko huku unaendelea kukoroga vizuri. Rudia hadi maziwa yote yachanganyike vizuri.
Paka chombo unachotumia kuokea mafuta na unga vizuri, kisha mimina mchanganyiko kwenye bakuli la kuokea. Weka kwenye oven. Tega oven dakika 45 hadi 50. Jaribu kama cake imeiva – ingiza kijiti au kitu chembamba, kisha toa. Kikitoka kikavu, keki imeiva, kikitoka kimelowa, acha cake kwenye oven kwa muda wa dakika 10 zaidi. Kisha jaribu.
Ukishatoa cake kwenye oven, unaweza kuipaka chocolate juu yake ili ivutie zaidi. Mie sikupaka chocolate, maana uwepo wa chocolate ulikuwa unatosha.
Hii cake unaweza kula kama kitafwa kawaida, muda wowote unapohitaji kutafuna kitu.
Kuandaa: dakika 15
Mapishi: dakika 60
Walaji: 8
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Mahitaji
Unga wa ngano vikombe 2
Sukari kikombe 1
Ndizi 2, zilizoiva vizuri
Mayai 2
Mafuta ya kula ½ kikombe (Au butter 2/3 kikombe)
Chumvi kijiko 1 kidogo
Kikombe 1½ cha maziwa
Baking soda kijiko 1 kidogo
½ kikombe cha cocoa ya kuokea (Au chocolate ya unga)
Vanilla flavor kijiko 1 kikubwa
Hii ni keki unayoandaa ukiwa na muda na hamu ya kula kitu kitamu, chenye afya na kinachoweza kukupa furaha. Ni muhimu kuandaa keki kama una muda mwingi wakati wa weekend, ili upate matokeo mazuri zaidi na kujumuika vizuri na familia.
Washa oven weka kwenye nyuzi 350°F (180°C). Acha ipate moto.
Kwenye bakuli kubwa, changanya butter na sukari hadi zichanganyike na kuwa laini. Ongeza mayai, moja baada ya jingine – pasua kisha changanya vizuri.
Kwenye chombo tofauti, changanya unga wa ngano, cocoa, vanilla flavor, baking soda na chumvi. Koroga vizuri. Changanya mchanganyiko huu kwenye bakuli lenye mchanganyiko wa mafuta na sukari. Kwenye chombo tofauti, ponda ndizi hadi zilainike vizuri kisha weka kwenye mchanganyiko wa unga na mafuta. Koroga vizuri.
Ongeza maziwa kidogo kwa wamu kwenye mchanganyiko huku unaendelea kukoroga vizuri. Rudia hadi maziwa yote yachanganyike vizuri.
Paka chombo unachotumia kuokea mafuta na unga vizuri, kisha mimina mchanganyiko kwenye bakuli la kuokea. Weka kwenye oven. Tega oven dakika 45 hadi 50. Jaribu kama cake imeiva – ingiza kijiti au kitu chembamba, kisha toa. Kikitoka kikavu, keki imeiva, kikitoka kimelowa, acha cake kwenye oven kwa muda wa dakika 10 zaidi. Kisha jaribu.
Ukishatoa cake kwenye oven, unaweza kuipaka chocolate juu yake ili ivutie zaidi. Mie sikupaka chocolate, maana uwepo wa chocolate ulikuwa unatosha.
Hii cake unaweza kula kama kitafwa kawaida, muda wowote unapohitaji kutafuna kitu.
Subscribe to:
Posts (Atom)
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...
-
JINSI YA KUPIKA CHAPATI LAINI MAANDALIZI/PREPARATION 1.Kwanza hakikisha unakanda unga vizuri Make sure you knead the dough very well...
-
MAHITAJI/INGREDIENTS 1.Nyama ya kusaga kilo kasorobo(3/4) 3/4 Kg Minced Meat 2.Kitunguu maji kikubwa 1 1 Medium size Onion 3.Ker...
-
Urojo ni mchanganyiko wa vyakula mbali mbali pamoja na uji uji wake katika bakuli moja. Hapa nitaeleza jinsi ya kuupika huo uji(urojo) m...
